Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 06/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 06/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 06/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

The Herald: Saratani ndio iliyomuua Mugabe

media Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uhai wake, wakati huo alitangaza kwamba hatakipigia kura chama cha Zanu-PF Julai 29, 2018. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, alikuwa anasumbuliwa na saratani, iliyosababisha kifo, mapema mwezi huu nchini Singapore.

Gazeti linalofadhiliwa na serikali nchini humo The Herald, limeripoti kuwa licha ya Mugabe kusumbuliwa na saratani kwa muda mrefu, afya yake ilianza kuwa mbaya baada ya kuondolewa madarakani na jeshi mwaka 2017.

Wakati wa uhai wake, Mugabe ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 alikuwa anakwenda mara kwa mara kupata matibabu nchini Singapore wakati huo, ikishukiwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na saratani ya tezi dume.

Rais Emmerson Mnangagwa akiwa jijini New York amenukuliwa na Gazeti la The Herald akiwaambia wafausi wa chama cha ZANU PF kuwa, madaktari walishindwa kuendelea kumpa matibabu Mugabe kwa sababu ya umri wake mkubwa lakini pia saratani ilikuwa imesambaa sana mwili na hivyo, matibabu yalikuwa hayasaidii.

Mugabe aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 37, anatarajiwa kuzikwa mwezi ujao katika makaburi ya mashujaa jijini Harare.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana