Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Felix Tshisekedi aendelea na ziara yake Ubelgiji kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili

media Rais wa DRC Felix Tshisekedi na mkewe Denise wanawasili Brussels, Ubelgiji kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu, Septemba 16, 2019. Benoit DOPPAGNE

Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi Tshilombo yupo jijini Brussels ikiwa ni ziara yake ya kwanza barani Ulaya tangu kuchaguliwa kwake katika uchaguzi uliogubikwa na utata.

Uhusiano wa Brussels na Kinshasa ulikuwa umefikia pabaya katika hatua za mwisho za utawala wa rais wa zamani Joseph Kabila na ziara hii inalenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Ziara ya rais Felix Tshisekedi nchini Ubelgiji ni ishara ya kuanza upya kwa uhusiano baina ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Ubelgiji, baada ya kutetereka katika dakika za mwisho za utawala wa rais Joseph Kabila.

Ikulu ya Kinshasa inasema huu ni ukurasa mpya uliofunguliwa, upande wa Ubelgiji wanasema hii ni ziara yenye ishara nzuri ambapo Ubelgiji inafurahishwa na hatua hiyo ya felix Tshisekedi kuzuru kwanza Brussels, Kabla ya Paris katika ziara yake hiyo ya kwanza barani Ulaya, ambapo mwanadiplomasia mmoja wa Ubelgiji amesikika akisema kwamba huu ni udhibitisho wa kudumisha uhusiano wa mataifa hayo mawili.

Hata hivyo baada ya ziara ya mjumbe na maafisa wa Ubelgiji mwezi Mei mwaka huu, hakuna hatua chanya iliopigwa katika uhusiano baina ya pande hizo mbili. Kile kinachotarajiwa kusainiwa hii leo Jumanne tayari kimekwisha jadiliwa, jumla ni mikataba minne ya makubaliano, pamoja na barua inayoashiria kurejea kwa mahusiano kati ya Kinshasa na Brussels.

Inatarajiwa kuona uhusiano wa kijeshi uliositishwa wakati wa utawala wa rais Joseph Kabila ukirejea, kufunguliwa upya kwa ubalozi mdogo wa Congo katika mji wa Anvers na kurejeshwa kwa shguhuli katika ubalozi mdogo wa Ubelgiji jijini Lubumbashi uliofungwa wakati wa mvutano. Leo Jumanne Tshisekedi atakutana na Waziri Mkuu wa Ubelgiji kwa mazungumzo rasmi kabla ya kukutana na mfalme wa Ubelgiji na baadae matajiri wa Ubelgiji.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana