Pata taarifa kuu
TANZANIA-UFARANSA

Tanzania yazindua mfumo mpya wa rada kuimarisha usalama wa anga

Nchi ya Tanzania hivi leo imezindua mfumo mpya wa rada ya kiraia ya kuongozea ndege katika viwanja vyake viwili kati ya vinne ambavyo na vyenyewe vitawekewa mfumo huo.

Jengo jipya la tatu la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere nchini Tanzania.
Jengo jipya la tatu la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere nchini Tanzania. Fredrick Nwaka
Matangazo ya kibiashara

Mfumo wa awali ulikuwa unauwezo wa kutazama asilimia 25 ya anga ya Tanzania huku kwa kiasi kikubwa ikitegemea rada za nchi jirani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa rada hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere, rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, amesema sasa nchi itakuwa salama na kwamba mashirika mengi ya ndege sasa yatavutiwa kutumia rada ya nchi yake.

00:33

John Pombe Magufuli SNIP Kuhusu Rada Mpya Tanzania 16SEPT2019 PAD

Rada nne zilizozinduliwa zina thamani ya fedha za Tanzania bilioni 67 na zimetengenezwa na kampuni ya kifaransa ya Thales Las France, ambapo mradi huu umefadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo, balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier, amesema kufungwa kwa rada hizi kunaonesha ushirikiano thabiti uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa, ambapo akaongeza kuwa nchi yake inaunga mkono juhudu za Serikali ya awamu ya tano nchini humo.

00:21

Frederick Clavier SNIP Kuhusu Rada Mpya Tanzania 16SEPT2019PAD

Rada nyingine zitafungwa katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, Mwanza na Songwe, ambapo zikikamilika, nchi hiyo itakuwa na uwezo wa kutazama anga lake lote kwa asilimia 100.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.