Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MUGABE-SIASA

Mwili wa Mugabwe kuonyeshwa kwenye maeneo ya kihistoria Zimbabwe

Mvutano unaendelea kati ya familia ya Robert Gabriel Mugabe na serikali kuhusu mahala atakapozikwa kiongozi huyo wa vita vya msituni alieongoza mapambano ya kukomesha utawala wa wazungu wachache katika nchi hiyo iliyokuwa inaitwa Rhodesia.

Mwili wa Mugabe umerejeshwa nchini Zimbabwe kwa mazishi yake ya kitaifa.
Mwili wa Mugabe umerejeshwa nchini Zimbabwe kwa mazishi yake ya kitaifa. © REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Mazishi yake yamepangwa kufanyika Jumapili Oktoba 15.

Mwili wa Robert Mugabe uliwasili Jumatano wiki hii jijini Harare, ambako ulipokelewa na Rais wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa na ujumbe kamili wa kijeshi.

Mwili wa Mugabwe utaonyeshwa kwenye maeneo ya kihistoria kwa siku kadhaa kabla ya kuzikwa mahala ambako bado hapajatangazwa, hii ikiashiria mvutano unaondelea bado kati ya familia ya kiongozi huyo wa zamani na serikali.

Mugabe, aliefariki akiwa na umri wa miaka 95 katika hospitali nchini Singapore, aliitawala Zimbabwe kuanzia uhuru mwaka 1980 hadi alipopunduliwa mwaka 2017.

Wakati wa utawala wake wa miaka 37, Zimbabwe iliporomoka kutoka taifa lililostawi hadi mgogoro wa kiuchumi.

Kuanzia leo Alhamisi, mwili wa Robert Mugabe utaonyeshwa kwenye Uwanja wa Rufaro, moja ya vitongozi vya mji wa Harare, ili kuruhusu raia kutoka maeneo mbalimbali nchini kuja kutoa heshima ya mwisho kwa shujaa maarufu wa vita vya ukombozi, "amesema Waziri wa Habari Monica Mutsvangwa.

Ni katika uwanja huo ndipo Robert Mugabe alichukuwa hatamu ya uongozi wa chi hiyo iliyokuwa ikiitwa Rhodesia, Aprili 18, 1980 chini ya utawala wa Wazungu, ukiongozwa na Ian Smith.

Mjane wake Robert Gabriel Mugabe, Grace Mugabe, amejifunika mtandio mweusi akiingizwa ndani ya gari.
Mjane wake Robert Gabriel Mugabe, Grace Mugabe, amejifunika mtandio mweusi akiingizwa ndani ya gari. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Baadaye leo Alhamisi alasiri, mwili wa Mugabe utapelekwa katika kijiji cha Zvimba, kilomita zaidi ya mia moja kutoka mji mkuu Harare, ambapo rais wa huyo wa zamani alikuwa na makazi.

Baadhi ya raia wa Zimbabwe wameshiriki katika sherehe ya kupokea mwili wa rais wa zamani, Robert Gabriel Mugabe ambaye alitimuliwa madarakani mwishoni mwa mwaka 2017 kwa mapinduzi ya jeshi.
Baadhi ya raia wa Zimbabwe wameshiriki katika sherehe ya kupokea mwili wa rais wa zamani, Robert Gabriel Mugabe ambaye alitimuliwa madarakani mwishoni mwa mwaka 2017 kwa mapinduzi ya jeshi. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Viongozi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Robert Gabriel Mugabe ikiwa ni pamoja na Rais wa China Xi Jinping, Rais wa zamani wa Cuba Raul Castro, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Mohammadu Buhari wa Nigeria na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.