Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MUGABE-SIASA

Zimbabwe: Robert Mugabe kuzikwa Septemba 15

Rais wa zamani wa Zimbabwe anatarajiwa kuzikwa Jumapili, Septemba 15 baada ya sherehe rasmi ambayo itafanyika Jumamosi. Hata hivyo familia ya Zimbabwe haijakubaliana na serikali sehemu ambapo atazikwa kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe.

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe.
Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe. AFP/Jekesai Njikizana
Matangazo ya kibiashara

Mwili wa Robert Mugabe utarejeshwa nyumbani Jumatano kutoka Singapore. Rais huyo wa zamani wa Zimbabwe anatarajiwa kuzikwa Jumapili (Septemba 15). Tangu Ijumaa, Rais Emmerson Mnangagwa ametangaza maombolezo ya kitaifa na kumpa mtangulizi wake hadhi ya "shujaa wa kitaifa", ambayo inampa nafasi kuzikwa katika "makaburi ya Mashujaa wa Taifa". Lakini familia ya rais haijajapendelea kiongozi wao kuzikwa katika makaburi hayo.

Leo Mugabe, mwipwa wa rais aliyetimuliwa madarakani Robert Gabriel Mugabe, alikutana na vyombo vya habari Jumamosi katika kijiji alikozaliwa Mugabe cha Kutama, kilometa 85 kutoka mji mkuu Harare, na kubaini kwamba tangu kiongozi kuang'atuliwa madarakani shujaa huyo wa zamani wa uhuru, hali yake ya afya iliendelea "kudhoofika". "Unaweza kufikiria watu ambao unaamini, watu ambao wanakulinda, watu ambao wanahusika na usalama wako, ndio wanaokuasi," amesema Leo Mugabe, mwipwa wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Leo Mugabe anasema hajui ni wapi mjomba wake alitaka kuzikwa. Lakini mazishi katika "makaburi ya Mashujaa wa Taifa", kama ilivyopangwa kabla ya kutimuliwa kwake madarakani, yatakuwa mazishi rasmi yaliyoandaliwa na aliyemuangusha Robert Mugabe, Emmerson Mnangagwa. Jambo ambalo litaleta shida kwa familia, ameongeza mwipwa wa Mugabe.

Katika makaburi hayo ndipo alizikwa mke wa kwanza wa Robert Gabriel Mugabe, Sally. Eneo ambalo lilijengwa kwa msaada wa Korea Kaskazini.

Sally, alikuwa mmoja wa wanaharakati wa ukombozi wa Zimbabwe, aliyetazamwa na wengi hadi kifo chake kama mama wa taifa la Zimbabwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.