Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Somalia yakabiliwa na baa la njaa

media Familia za watu kutoka Somalia katika kambi ya wakimbizi kusini mashariki mwa Ethiopia. Picha ya tarehe 27 Januari, 2018. © AFP/YONAS TADESSE

Wanaharakati wa haki za binadamu wanatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchangia ili kuepuka janga lingine nchini Somalia. Kulingana na Umoja wa Mataifa, ikiwa misaada hautoimarishwa haraka, zaidi ya watu milioni mbili wako katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa ifikapo mwezi Desemba.

Kiwango cha tahadhari kiko kwenye alama nyekundu. Msimu wa mvua uliopita ulikuwa mbaya na mavuno ya nafaka si mazuri tangu mwaka 2011 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula (FAO).

Kama matokeo, watu wasiopungua milioni mbili wako katika hatari kubwa ya kukumbwa na baa la nja ifikapo mwezi Desemba. Kwa yote hayo, hadi mwishoni mwa mwaka huu, Wasomalia zaidi ya milioni sita watapata maradhi ya utapiamlo, sawa na karibu nusu ya idadi ya wakaazi wa Somalia.

Hali hii inatokana na mtikisiko wa tabia nchi.

Rais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia ameitaka jamii ya kimataifa kutuma misaada ya dharura katika maeneo yanayokabiliwa na ukame na baa la njaa nchini humo.

Rais huyo amewataka Wasomali waishio nje ya nchi kuwajali ndugu zao wanaokabiliwa na njaa na kiu kutokana na ukame unaoitafuna nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Rais wa Somalia amesema msimu wa masika umepita pasina kushuhudiwa mvua zozote nchini humo, hivyo maeneo mengi yanakabiliwa na ukame. Ameitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati na kutuma misaada ya dharura katika maeneo hayo kabla hali haijawa mbaya zaidi.

Mpango wa kibinadamu wa miezi sita, wenye thamani ya dola Milioni 487, ulizinduliwa mnamo mwezi Juni. Lakini mpaka sasa michango hiyo haijafikia hata nusu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana