Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-WAGENI-UVAMIZI-FUJO-BIASHARA

Vijana wengi nchini Afrika Kusini hawaelewi historia ya nchi yao

Utafiti kutoka kwa taasisi ya wahamiaji Kusini mwa Afrika, Southern African Migration Project (SMAP), unaonesha kuwa, visa vya kiraia wa kigeni kuvamiwa nchini Afrika Kusini, vinaendelea kuongezeka.

Afisa wa zima moto akiokoa duka la raia wa kigeni jijini Johannerburg kutokana na uvamizi dhidi ya maduka ya wageni.
Afisa wa zima moto akiokoa duka la raia wa kigeni jijini Johannerburg kutokana na uvamizi dhidi ya maduka ya wageni. REUTERS/Marius Bosch
Matangazo ya kibiashara

Historia inaonesha kuwa, tangu uongozi wa watu weusi kuingia madarakani mwaka 1994 baada ya kumalizika kwa mapambano ya ubaguzi wa rangi.

Kabla ya mwaka 1994, wahamiaji kutoka mataifa mengine waliokuwa wanaoshi nchini Afrika Kusini, walikuwa wanakumbana na ubaguzi na hata kushambuliwa.

Ilitarajiwa kuwa, baada ya kuingia madarakani kwa watu weusi, mauaji, uvamiizi na usumbufu kwa wangeni ungepungua lakini kwa bahati mbaya , jambo hili limeongezeka na halionekani kupata ufumbuzi.

Kati ya mwaka 2000 hadi 2008 watu 67 waliuawa katika mashambulizi dhidi ya wageni, lakini pia wakiwemo wenyeji zaidi ya 20, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na jeshi la Polisi nchini humo.

Mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka 2019, raia wa nchi hiyo walikuwa wamejihami kwa mapanga na mashoka, walivamia maduka ya raia wa kigeni wengi wao kutoka Nigeria jijini Johannesrburg.

Polisi waliripoti mauaji ya watu watano, huku wengine zaidi ya 100 wakikamatwa.

Hali kama hii pia iliwahi kuripotiwa mwezi Machi mwaka 2019 ambapo maduka ya wageni jijini Durban yalivamiwa na bidhaa kuibiwa.

Idadi kubwa ya raia wanaoishi nchini Afrika Kusini, ni kutoka nchi jirani ya Zimbabwe, Msumbiji, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Nini chanzo cha mashambulizi dhidi ya wageni ?

Mwaka 2018, kituo cha utafiti cha Pew, ilitoa ripoti iliyoeleza kuwa asilimia 62 ya raia wa Afrika Kusini, wanaona kuwa wageni ni mzigo kwao kwa sababu wanachukua kazi zao.

Aidha, utafiti huo, ulionesha kuwa asilimia 61 ya raia wa nchi hiyo waliamini kuwa wageni ndio wanaosababisha ongezeko la uhalifu nchini humo.

Imebainika kuwa kati ya mwaka 2010 hadi 2017, idadi ya wahamiaji nchini Afrika Kusini imeongeza kutoka Milioni 2 na kufikia Milioni 4.

Idara ya serikali inayoshughulikia takwimu, inaonesha vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 ambao ni asilimia 55.2 ya watu nchini humo, hawana ajira.

Aidha, kwa kipindi cha mwaka wa kwanza 2019, kiwango cha ukosefu wa ajira hasa kwa vijana ni asilimia 59.3.

Hatua zinazochukuliwa

Jeshi la Polisi nchini humo, linasema uvamizi huu ni uhalifu, na imekuwa ikiendelea kuzuia uvamizi huu.

Rais Cyril Ramaphosa amelaani uvamizi dhidi ya wageni na kusema kinachoendelea hakikubaliki.

“Nataka hili limalizike, kwa sababu hakuna sababu ya raia wa kigeni wanaofanya biashara kuvamiwa,” alisema.

Mwezi Machi, serikali ya Afrika Kusini, ilizindua mpango kazi wa kupambana na suala hili na ikapendekezwa kuwa kupambana na machafuko kama haya, serikali ipambane na umasikini na kupunguza mwanya kati ya wale walichonacho na wasichonacho.

Aidha, vijana wa Afrika Kusini wanahitaji kupata elimu ya historia kuhusu nchi yao na kuachana na itikadi za kikoloni.

Rais wa zamani wa Ghana John Mahama wakati mmoja aliwahi kusema, vijana wa Afrika Kusini hawafahamu historia ya nchi yao, namna mataifa ya bara la Afrika walivyosimama na nchi yao.

Mataifa ya kigeni, yamelaani machafuko haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.