Pata taarifa kuu
DRC-UN-USALAMA

Guterres atoa wito kwa MONUSCO na jeshi la DRC kudumisha ushirikiano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress ametembelea mjini Beni Mashariki mwa DRC na kuahidi kuwa Umoja wa Mataifa kupitia jeshi la kulinda amani, litaendelea kulisaidia jeshi la nchi hiyo, kupambana na makundi ya waasi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwasili Beni, mashariki mwa DRC, Septemba1, 2019.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwasili Beni, mashariki mwa DRC, Septemba1, 2019. ALEXIS HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Guteress ametoa kauli hii, ikiwa ni siku yake ya pili akiwa nchini DRC, baada ya kuwasili nchini humo siku ya Jumamosi kwenda kujionea jitihada zinazofanyika kupambana na ugonjwa hatari wa Ebola lakini pia vita dhidi ya waasi.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema jeshi la MONUSCO litaendelea kushirikiana na maafisa wa usalama nchini humo jeshi na polisi, kuhakikisha kuwa usalama na amani zinarejea katika Wilaya ya Beni.

Wilaya ya Beni, imeendelea kusumbuliwa na waasi, hasa wa ADF Nalu ambao mara kwa mara wameendelea kuwashambulia raia wasiokuwa na hatia.

Mashambulizi ya waasi hayo pia yameelezwa kurudisha nyuma, juhudi za kupambana na Ebola, kutokana na visa vya kuvamiwa kwa maafisa wa afya wanaotoa huduma muhimu kwa walioathiriwa.

Mbali na suala la usalama, Guteress pia amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kupambana kuhakikisha kuwa Ebola inakomeshwa.

Tangu mwezi Agosti mwaka 2018, Ebola imesababisha vifo vya watu zaidi ya 2,000 na wengine zaidi ya elfu tatu wakiambukizwa, huku eneo lililoathiriwa zaidi likiwa ni Beni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.