Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Guteress azuru Beni, aahidi MONUSCO kuendelea kupambana na waasi

media Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress akiwa na baadhi ya wapiganaji wa zamani waliondoka kwenye makundi ya waasi, baada ya kuzuru mjini Beni Mashariki mwa DRC MONUSCO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress ametembelea mjini Beni Mashariki mwa DRC na kuahidi kuwa Umoja wa Mataifa kupitia jeshi la kulinda amani, litaendelea kulisaidia jeshi la nchi hiyo, kupambana na makundi ya waasi.

Guteress ametoa kauli hii, ikiwa ni siku yake ya pili akiwa nchini DRC, baada ya kuwasili nchini humo siku ya Jumamos,i kwenda kujionea jitihada zinazofanyika kupambana na ugonjwa hatari wa Ebola lakini pia vita dhidi ya waasi.

Mkuu huyo wa UN amesema jeshi la MONUSCO litaendelea kushirikiana na maafisa wa usalama nchini humo jeshi na polisi, kuhakikisha kuwa usalama na amani zinarejea katika Wilaya ya Beni.

Wilaya ya Beni, imeendelea kusumbuliwa na waasi hasa wa ADF Nalu ambao mara kwa mara wameendelea kuwashambulia raia wasiokuwa na hatia.

Mashambulizi ya waasi hayo pia yameelezwa kurudisha nyuma, juhudi za kupambana na Ebola, kutokana na visa vya kuvamiwa kwa maafisa wa afya wanaotoa hudumu muhimu kwa walioathiriwa.

Mbali na suala la usalama, Guteress pia amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kupambana kuhakikisha kuwa Ebola inakomeshwa.

Tangu mwezi Agosti mwaka 2018, Ebola imesababisha vif vya watu zaidi ya 2,000 na wengine zaidi ya elfu watu wakiambukizwa, huku eneo lililoathiriwa zaidi likiwa ni Beni.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana