Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Wananchi wa Sudani waendelea kusubiri serikali mpya baada ya Bashir

media Waziri Mkuu wa mpito wa Sudani Abdallah Hamdok wakati wa shereheya kuapishwa kwake, Khartoum Agosti 21, 2019. Ebrahim HAMID / AFP

Waziri Mkuu wa Sudani Abdallah Hamdok amechelewesha kutangazwa kwa serikali ya kwanza nchini Sudani tangu rais Omar al-Bashir kutimuliwa madarakani, ili kuweza kuendelea na majadiliano kuhusu uteuzi wa mawaziri wake, amesema afisa mmoja nchini Sudani.

Serikali hii mpya inatarajiwa kukabiliwa na changamoto kubwa baada ya miongo mitatu ya utawala wa kijeshi na miezi kadhaa ya maandamano yaliyopelekea jeshi kumtimua na kumkamata aliyekuwa rais wa nchi hiyo Omar Hassan al-Bashir.

Kulingana na makubaliano ya kihistoria yaliyosainiwa Agosti 17 kati ya viongozi wa waandamanaji na wanajeshi, serikali mpya ilitarajiwa kutangazwa Jumatano wiki hii.

Lakini tangazo hilo lilicheleweshwa kwa sababu "majadiliano juu ya uteuzi wa mawaziri bado yanaendelea," kilisema chanzo kilio karibu na Hamdok, aliyetawazwa Agosti 21. Chanzo hiki hakijabainisha ni lini serikali mpya itatangazwa.

Waziri mkuu anatarajia kuteua wajumbe wa baraza lake la mawaziri kati ya majina yaliyopendekezwa na vuguvugu la Uhuru na Mabadiliko (FLC), kundi la wanarakati walioanzisha maandamano nchini Sudani.

- "Amani ya kudumu" -

Serikali inapaswa kuundwa na jumla ya mawaziri 20, walioteuliwa na Bwana Hamdok isipokuwa Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Ulinzi, ambao watateuliwa na askari wanaojumuika kwenye Baraza Kuu Tawala.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana