Pata taarifa kuu
AFRIKA-JAPANI-USHIRIKIANO

Mkutano kati ya Afrika na Japani kufunguliwa Jumatano hii

Viongozi kadhaa wa Afrika wanatarajia kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa saba wa TICAD mjini Yokohama, Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe wakati wa mkutano wa G20, Osaka, Juni 28, 2019 (picha ya kumbukumbu).
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe wakati wa mkutano wa G20, Osaka, Juni 28, 2019 (picha ya kumbukumbu). © Ludovic MARIN / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa kilele wa TICAD ulioandaliwa na Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia ni fursa kwa Japan kuonyesha tofauti na jirani yake kubwa, China, ambayo imekuwa moja ya wawekezaji wakubwa barani Afrika katika muongo mmoja.

Katika kiezi ya hivi karibuni, Rais wa China Xi Jinping alizitaka nchi zaidi duniani zijiunge na mradi wa nchi yake wa ujenzi wa miundombinu, mpango ambao Marekani inahofia unajenga ushawishi mkubwa zaidi wa kimkakati kwa manufaa ya China.

Mwishoni mwa mwezi Juni nchi za kiafrika ziliomba China kuhakikisha kuwa ufadhili ama mikopo inayotoa kwa nchi za kiafrika inalenga katika miradi ya kikanda itakayoziunganisha na kuzinufaisha nchi hizo kiuchumi.

China imekuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika, ikijihusisha kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa reli katika mataifa ya Kenya na Ethiopia. Hata hivyo wakosoaji wa uwekezaji unaofanywa na China barani Afrika wanasema unaongeza madeni kwa mataifa ya Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.