Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Kesi ya Omar al-Bashir: Upande wa utetezi waomba mteja wao aachiliwe kwa dhamana

media Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir akisikilizwa mahakamani Khartoum Agosti 24, 2019. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Rais wa zamani wa Sudani Omar Hassan al-Bashir, amekana mashtaka dhidi yake, timu yake ya utetezi, inayoundwa na wanasheria 96, ina matumaini kuwa mteja wao ataachiliwa kwa dhamana.

Rais wa zamani wa Sudani Omar al-Bashir alifikishwa mahakamani Jumamosi, huku akitabasamu. Hii ni mara ya pili kesi yake ya ufisadi inasikilizwa mahakamani Khartoum. Hata hivyo wanasheria wake wameomba achiliwe kwa dhamana.

Kesi ya kiongozi huyo wa zamani wa Sudan, iliyowasilishwa na jeshi Aprili 11 baada ya miaka thelathini madarakani, ilifunguliwa Agosti 19. Anakabiliwa na mashtaka ya "kumiliki fedha za kigeni, ufisadi" na kutumia madaraka vibaya.

Agosti 19, mchunguzi mmoja alidai kwamba Omar al-Bashir alikiri kupokea pesa nyingi kutoka Saudi Arabia kwa pesa taslimu kiasi cha dola milioni 90 (sawa na euro milioni 80).

Siku ya Jumamosi, jaji alisikiliza mashahidi watatu, ikiwa ni pamoja na wachunguzi wawili ambao walifanya ukaguzi kwenye makazi yake na kupata pesa nyingi.

Kwa upande wake, upande wa utetezi umeomba rais wa zamani wa Sudani aachiliwe kwa dhamana. "Tunaomba mahakama imuachilie kwa dhamana mtuhumiwa," amesema mwanasheria wake Hashem Abu Bakr.

Jaji amejibu kwamba atatathmini ombi hilo na kutangaza kwamba kesi itasikilizwa tena Agosti 31.

Baada ya kusikilizwa, Omar Hassan al-Bashir amerejeshwa gerezani, wakati huo huo makundi mawili yaliandamana karibu na mahakama, shirika la habari la AFP limebaini.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana