Pata taarifa kuu
DRC-MAWAZIRI-RAIS-TSHISEKEDI

Baraza la Mawaziri nchini DRC kutangazwa wakati wowote

Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado wanasubiri Baraza jipya la Mawaziri karibu miezi minane tangu kuingia madarakani kwa rais Félix Tshisekedi mapema mwaka 2019.

Waziri Mkuu mpya wa DRC Sylvestre Ilunga Ilukamba (Kushoto) akisalimiana na rais Felix Tshisekedi (Kulia) walipokutana jijini Kinshasa Mei 20 2019
Waziri Mkuu mpya wa DRC Sylvestre Ilunga Ilukamba (Kushoto) akisalimiana na rais Felix Tshisekedi (Kulia) walipokutana jijini Kinshasa Mei 20 2019 www.rfi.fr
Matangazo ya kibiashara

Baraza hilo lilitarajiwa kutajwa wiki hii na Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga, lakini inavyoonekana, raia wa DRC watasubiri kwa saa kadhaa,  siku moja au mbili zaidi kabla ya kutangazwa.

Ripoti kutoka Kinshasa zinasema kuwa, rais Tshisekedi ametaka baraza hilo kupunguzwa kwa nafasi mbili na huenda sasa serikali ikatangazwa wakati wowote kuanzia Jumatatu wiki ijayo.

Waziri Mkuu Ilunga amesema kuwa, zoezi hilo linachukua muda mrefu kwa sababu maeneo yote ya DRC yanastahili kuwakilishwa katika baraza hilo ambalo litaundwa na wanasiasa kutoka upande wa rais Tshisekedi na rais wa zamani Joseph Kabila.

Katika siku zilizopita, kumekuwa na maandamano jijini Kinshasa kutoka kwa wananchi wakihoji ni kwanini imechukua muda mrefu kutangaza majina ya Mawaziri wapya.

Kazi kubwa la serikali mpya inayosubiriwa kwa hamu, kwanza ni kuimarisha usalama Mashariki mwa DRC , kupambana na ugonjwa wa Ebola na kuimarisha maisha ya raia wa nchi hiyo wanaoendelea kuishi kwa umasikini mkubwa licha ya nchi hiyo kuwa na rasilimali nyingi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.