Pata taarifa kuu
GABON-RFI-VYOMBO VYA HABARI

Gabon yamsimamisha mwandishi wa RFI kufanya kazi kwa muda wa miezi miwili

Mamlaka ya juu ya Mawasiliano nchini Gabon imetangaza jana usiku kwenye runinga kuwa mwandishi wetu Yves-Laurent Goma amepigwa marufuku kwa miezi miwili kufanya kazi yake kama mwandishi wa habari nchini humo kuanzia Alhamisi wiki hii.

Studio ya RFI
Studio ya RFI © RFI
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja kutokana na kwamba mwandishi huyo wa habari aliripoti kwa RFI katika makala yaliyochapishwa Agosti 17 kwamba "Rais wa Gabon Ali Bongo hajawahi kusimama na kusalimia jeshi kama ilivyokuwa wakati wa nyuma." Mamlaka ya Juu ya Mawasiliano imelaani "habari isiyo sahihi ambayo inaonesha picha mbaya na kumkejeli Rais wa Jamhuri Ali Bongo".

Uongozi wa RFI umeelezea masikitiko yake dhidi ya hatua hiyo ya Mamlaka ya Juu ya Mawasiliano nchini Gabon ya kusimamisha kibali cha Yves-Laurent Goma cha kufanyia kazi za uandishi wa habari kwa muda wa miezi mbili.

RFI imebaini kwamba msimamo wake unaendana na uhuru wa habari na inataka mwandishi wake apate kibali cha kufanya kazi haraka iwezekanavyo ili aendelee kutoa habari kuhusu Gabon, kama alivyo kuwa akifanya kwa kipindi chote hicho cha miaka 17.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.