Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA

Sudani: Rais na wajumbe wa Baraza Kuu Tawala watawazwa rasmi

Kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia nchini Sudan, kufuatia mkataba wa kihistoria kati ya jeshi na viongozi wa maandamano, kimeanza Jumatano hii, Agosti 21 na kwa kutawazwa kwa rais wa Baraza Kuu Tawala .

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akitawazwa kama rais wa Baraza Kuu Tawala Sudan, Khartoum Agosti 21, 2019.
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akitawazwa kama rais wa Baraza Kuu Tawala Sudan, Khartoum Agosti 21, 2019. © SUDAN PRESIDENTIAL PALACE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais mpya wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ameapishwa mbele ya mamlaka ya juu zaidi nchini humo. Wajumbe wengine kumi wa Baraza Kuu Tawala wamekula kiapo mbele ya rais. Uteuzi rasmi wa waziri mkuu unatarajiwa leo kufanyika baadaye leo jioni.

Chini ya masharti ya mkataba wa kisiasa uliyotiwa saini Jumamosi, Agosti 17, Abdel Fattah al-Burhan ataongoza Sudan kwa kipindi cha miezi ishirini na moja, kabla ya kukabidhi madaraka kwa raia ambaye ataongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miezi kumi na nane kitakacho salia.

Majina ya raia miongoni mwa wajumbe wa Baraza Kuu Tawala yalitangazwa Jumanne Agosti 20 jioni.

Taasisi hii mpya inaundwa na raia sita na askari watano. Baraza hilo KUu Tawala linajumuisha wanawake wawili lakini pia askari wa utawala wa zamani. Baraza hilo litasimamia mchakato wa kuundwa kwa Serikali na Bunge la Mpito.

Kuhusu Waziri Mkuu mpya, Abdallah Hamdok, anatarajia kula kiapo leo Jumatano usiku. Atakuwa na kibarua cha kuunda haraka serikali kabla ya Agosti 28. Mkutano wa kwanza kati ya Baraza Kuu Tawala na serikali umepangwa kufanyika tarehe 1 Septemba mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.