Pata taarifa kuu
SUDAN-SERIKALI-MAANDAMANO

Serikali ya mpito nchini Sudan kutajwa, kuongoza miaka mitatu

Uongozi wa kijeshi na kiraia utakaongoza Sudan unazinduliwa siku ya Jumanne, jijini Khartoum baada ya mkataba utakaotoa mwongozo wa serikali hiyo kutiwa saini hivi karibuni.

Viongozi wa serikali ya mpito nchini Sudan baada ya kutia saini mkataba wa serikali Agosti 17 2019
Viongozi wa serikali ya mpito nchini Sudan baada ya kutia saini mkataba wa serikali Agosti 17 2019 AFP/Ebrahim HAMID
Matangazo ya kibiashara

Serikali hii ya mpito ambayo ilitarajiwa kutangazwa siku ya Jumapili iliyopita, iliahirishwa hadi wiki hii kwa mujibu wa taarifa za kijeshi.

Serikali hii itaongoza nchi hiyo kwa kipindi hicho, baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani Omar Al Bashir mwezi Aprili, kufuatia maandamano ya wananchi.

Mbali na wanajeshi, serikali hiyo inaundwa na viongozi wa waandamanaji na vikundi vya upinzani.

Baraza la juu litakaloongoza, litakuwa na wajumbe 11, sita kutoka upande wa kiraia na wengine watano upande wa kijeshi.

Uongozi huo wa juu, utasimamia uteuzi wa Baraza la Mawaziri wakiwemo wabunge wakataowakilisha raia wa nchi hiyo.

Awamu ya kwanza ya uongozi wa serikali itaongozwa na Jenerali wa kijeshi kwa kipindi cha miezi 21 huku kiongozi wa kiraia akimalizia awamu ya pili ya miezi 18.

Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika nchini humo, baada ya kumalizika kwa serikali hiyo ya mpito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.