Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Watatu wauawa kwa kupigwa risasi katika maandamano ya kupinga ukosefu wa usalama Beni

Watu watatu wameuawa leo Jumatatu, Agosti 19 kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya kupinga ukosefu wa usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo visa vya mauaji vimekithiri, kwa mujibu wa vyanzo rasmi.

Wilaya ya Beni, Mkoa wa Kivu Kaskazini, DR Congo: vikosi vya Umoja wa Mataifa (MONUSCO)kwa ushirikiano na majeshi ya DRC (FARDC) katika operesheni inayoitwa usalama.
Wilaya ya Beni, Mkoa wa Kivu Kaskazini, DR Congo: vikosi vya Umoja wa Mataifa (MONUSCO)kwa ushirikiano na majeshi ya DRC (FARDC) katika operesheni inayoitwa usalama. Photo MONUSCO/Force
Matangazo ya kibiashara

"Kulikuwa na maandamano ambapo watu watatu wameuawa: mvulana mdogo wa takriban miaka 25 ambaye amepigwa risasi tumboni, amefariki baada ya kufikishwa hospitalini; na mtu mwengine kutoka jamii ya Mamburikimo amepigwa risasi, na kufariki papo hapo; mtoto mwingine pia amepigwa risasi na kufaruki duni, "Donat Kibwana, Mkuu wa wilaya ya Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini, ameliambia AFP shirika la habari la AFP.

Hali ya usalama katika eneo hilo la Mashariki mwa DRC, si shwari. Usalama umekuwa ukidorara kila mara, huku visa vya mauaji vikiendelea kuongezeka.

Kundi la waasi wa Uganda la ADF limekuwa likinyooshewa kidole cha lawama kwamba linahusika na mauaji hayo.

Lakini wadadisi wanaesema kwamba kundi hlo limekuwa likishirikiana na makundi mengine ya raia wa DRC wanaobebelea silaha kwa kuzorotesha usalama katika eneo hilo.

Makundi hayo yameendelea kunufaika na vitendo hivyo hasa kwa kupora mali za raia na mali asili ya nchi hiyo hasa madini na kuyauza katika nchi jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.