Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Sudani: Kesi ya rushwa dhidi ya Omar al-Bashir yafunguliwa Khartoum

media Rais wa Sudan aliye timuliwa mamlakani Omar al-Bashir akiwa kizimbani wakati wa ufunguzi wa kesi yake ya ufisadi, Khartoum, Agosti 19, 2019 © Ebrahim HAMID / AFP

Omar Hassan al-Bashir ambaye alitimuliwa mamlakani Aprili 11 baada ya miezi minne ya maandamano ya raia nchini Sudani, ametakiwa kujibu mashitaka ya rushwa yanayomkabili.

Kesi inayomkabili Bw Bashir ilitarajiwa kuanza kusikilizwa Jumamosi, Agosti 17, lakini iliahirishwa mara moja, kutokana na tukio la kusainiwa kwa mkataba wa kugawana madaraka kati ya raia na jeshi ambalo lilipangwa kufanyika siku hiyo hiyo.

Mashtaka dhidi ya rais huyo wa zamani ni pamoja na"kumiliki fedha za kigeni" na vitendo vya "hongo," kwa mujibu wa upande wa mashtaka.

Itakumbukwa kuwa muda mfupi baada ya kukamatwa kwake, viongozi wa jeshi la mpito waliamuru dola bilioni 113 zilizokamatwa nyumbani kwa Omar Hassan al-Bashiri zionyesgwe kwenye televisheni ya serikali. Mwezi Juni, mmoja wa mawakili wake alisema pesa hizo ni "fedha za dharura", ambazo ni, akiba inayowekwa mikononi mwa rais ili kukabiliana na hali ngumu.

Mchunguzi anayeshughulikia kesi hiyo ameilezea mahakama kuwa dola milioni 90 ilikuwa ni zawadi kutoka kwa mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohamed Ben Salmane.

Baada ya Omar al-Bashir kukamatwa Aprili mwaka jana, mwendesha mashtaka pia alibaini kwamba Omara Hassan al-Bashir anakabiliwa mashtaka ya "mauaji" ya waandamanaji, lakini bila kutoa maelezo zaidi.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana