Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Sudani: Waziri Mkuu mpya Abdalla Hamdok kuthibitishwa Agosti 20

media Jenerali Hamdan Daglo, Naibu Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito, na Ahmed Rabie, Kiongozi wa maandamano, Khartoum Agosti 4, 2019. © ASHRAF SHAZLY / AFP

Waziri Mkuu mpya nchini Sudani atatangazwa hivi karibuni. Jina lake limepitishwa Alhamisi, Agosti 15 na wawakilishi wa waandamanaji ambao walitakiwa kutoa jina la mtu atakayeshikilia nafasi hiyo.

Waziri huyo mkuu mpya wa Sudan anaitwa Abdalla Hamdok na atathibitishwa Jumanne, Agosti 20 na Baraza Kuu la uongozi wa nchi, ambalo ni taasisi mpya la mpito.

Abdalla Hamdok, ambaye ni mchumi mbobezi alishikilia wadhifa wa naibu katibu wa Tume ya Uchumi ya Afrika katika Umoja wa Mataifa hadi mwaka jana.

Aliteuliwa bila kupingwa Alhamisi kuongoza serikali ya mpito ijayo nchini Sudani. Serikali ambayo raia watakuwa na nafasi muhimu kwani raia watapewa wizara 18. Jeshi litakuwa na wizara mbili tu, Ulinzi na Mambo ya Ndani.

Uchaguzi wa Abdalla Hamdok unatarajiwa kupitishwa rasmi Jumanne ya wiki ijayo. Uamuzi wa mwisho utatoka kwa Baraza Kuu, ambalo litaongoza katika kipindi chote cha mpito nchi hiyo.Taasisi hiyo inatarajiwa kuundwa Jumapili hii, Agosti 18, siku moja baada ya hafla ya kutiwa saini kwa makubaliano ya jumla yanayoweka masharti ya kipindi cha mpito na kugawana madaraka kati ya raia na jeshi.

Makubaliano hayo yalipatikana katika wiki za hivi karibuni baada ya miezi nane ya mvutano na machafuko ambayo yaligharimu maisha ya watu zaidi ya 250 upande wa waandamanaji. Makubaliano hayo pia yanatoa nafasi ya kuundwa kwa "Kamati ya Uchunguzi Huru" ili wahusika wa vitendo hivyo wawajibishwe.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana