Pata taarifa kuu

Helikopta mbili aina ya "Puma" zazua maswali mengi Mali

Serikali ya Mali inaendelea kulaumiwa kuhusu helekopta mbili ilizopata ambazo hazijaweza kupaa angani tangu zilipowasili nchini humo.

Kwa upande wa Rais Ibrahim Boubacar Keïta (picha ya kumbukumbu), kuna "tatizo la kiufundi " upande wa helikopta hizi mbili aina ya "Puma" zilizonunuliwa na Mali.
Kwa upande wa Rais Ibrahim Boubacar Keïta (picha ya kumbukumbu), kuna "tatizo la kiufundi " upande wa helikopta hizi mbili aina ya "Puma" zilizonunuliwa na Mali. © RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwaka 2017, Mali ilipata helikopta mbili kwa jeshi lake la anga, kupambana dhidi ya wanamgambo wa kiislamu.

Helikopta hizo mbili aina ya "Puma" ilikuwa miongoni mwa vifaa ilivyopata. Lakini kwa miezi kadhaa, helikopta hizo haizajapaa angani, kutokana na, "suala la matengenezo," kwa mujibu wa Rais Ibrahim Boubacar Keita mwenyewe.

Karim, mtoto wa Rais wa Mali na mbunge wa Bunge la taifa nchini humo, amehoji ikiwa Mali haikutapeliwa wakati wa kununua helikopta hizo mbili.

Kwa upande wake, waziri wa mawasiliano na msemaji wa serikali ya Mali Yaya Sangaré, hivi karibuni aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba "ukweli utajulikana na mambo yote yatawekwa wazi kuhusu kesi hiyo"; hatua kali zitachukuliwa.

Helikopta hizo mbili aina ya Puma zilizonunuliwa baada ya kutumika ziliwasili nchini Mali mnamo mwaka 2017, wakati huo ziliwasili nchini zikipaa angani. Rais Ibrahim Boubacar Keita (IBK) alikuwepo hata kwenye sherehe rasmi ambapo ndege zilikuwa zikipaa angani zikifanya maonyesho angani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.