Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 10/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mkataba wa kusitisha mapigano wavunjwa Libya

media Uwanja wa ndege wa Mitiga, uliolengwa na roketi, Jumapili, Agosti 11. (Picha ya tarehe 8 Aprili, 2019). © Mahmud TURKIA / AFP

Mapigano makali kati ya makundi hasimu nchini Libya yamelenga uwanja wa ndege wa Mitiga, jana Jumapili, uwanja pekee unaofanya kazi katika mji mkuu wa Libya, Tripoli na kukiuka mkataba wa muda wa kusitisha mapigano yaliyokua yakienelea kwa miezi minne kando ya mji wa Tripoli.

Uwanja wa ndege wa Mitiga unapatikana kilomita kadhaa na eneo linalodhibitiwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNA), yenye makao yake makuu mjini Tripoli.

"Uwanja wa ndege wa Mitiga ulishambuliwa kwa risasi asubuhi ya siku ya kwanza ya Eid al-Adha," Mamlaka ya uwanja wa ndege imeandika kwenye ukurasa wake wa Facebook. Safari za ndege zimesitishwa, mamlaka ya uwanja wa ndege wa Mitiga imeongeza.

Mbabe wa kivita mashariki mwa Libya, Marshal Khalifa Haftar alizindua mapigano tarehe 4 Aprili kwa lengo la kudhibiti mji wa Tripoli, makao makuu ya serikali ya Umoja wa Kitaifa inayotambuliwa na Uoja wa Mataifa.

Baada ya zaidi ya miezi minne ya mapigano mabaya, vikosi vya Marshal vinaendelea kupiga kambi nje ya mji mkuu, vikizuiliwa na vikosi vya serikali ya Umoja wa Kitaifa GNA.

Makundi hasimu katika mgogoro huo wa Libya yameendelea kushtumiana kila upande kukiuka mkataba wa muda wa kusitisha mapigano ulioombwa na Umoja wa Mataifa wakati wa kusherehekea siku kuu ya Eid al-Adha, maadhimisho ya kidini ambayo yalianza Jumapili na yanaendelea hadi Jumanne nchini Libya.

"Wanamgambo wa Haftar wamekiuka mkataba huo mara mbili," msemaji wa vikosi vya serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNA), Moustafa al-Mejii ameliambia shirika la habari la AFP. "Mara ya kwanza mashambulizi ya wanamgambo hao yalilenga makaazi huko Soug al-Jomaa (mashariki mwa Tripoli), na kuwajeruhi raia watatu, na mara ya pili kwa kushambulia uwanja wa ndege wa Mitiga," Moustafa al-Meiji ameshtumu.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumapili jioni, Umoja wa Falme za Kiarabu, Marekani, Ufaransa, Italia na Uingereza zilitaka pande husika kuheshimu mkataba wa muda wa kusitisha mapigano na kuyataka makundi hayo hasimu "kumaliza uhasama katika nchi nzima ya Libya."

Nchi hizo tano zimetoa wito kwa "pande zote kufikira mkataba wa kusitisha mapigano bila kuchelewa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana