Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Barua pepe zilizovuja zamuweka mashakani Ramaphosa

media Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anaendelea kupinga ripoti ya ofisi ya msimamizi wa mali za umma ambayo ilimtaja kudanganya bunge kuhusu kupokea fedha za michango kusaidia kampeni yake mwaka 2017. REUTERS/Rodger Bosch

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza kuwa hana kosa lolote baada ya kuvuja kwa barua pepe kuhusu mchango aliopokea wakati wa kampeni ndani ya chama cha ANC mwaka 2017.

Mwishoni mwa mwezi Julai rais Cyril Ramaphosa alisema ataenda mahakamani kupinga ripoti ya ofisi ya msimamizi wa mali za umma ambayo ilimtaja kudanganya bunge kuhusu kupokea fedha za michango kusaidia kampeni yake mwaka 2017.

Kwenye ripoti hiyo Ramaphosa anadaiwa kupokea kiasi cha randi laki 5 kusaidia kampeni zake kinyume na maadili ya utumishi wa uma.

Tayari mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi wa mali za uma, Busisiwe Mkhwebane ametoa taarifa akiunga mkono hatua iliyochukuliwa na rais Cyril Ramaphosa.

Awali Ramaphosa aliesema baada ya kuisoma kwa kina alibaini kuwa ripoti hiyo ina makosa na tuhuma za kupikwa na kutaka mara moja ifanyiwe mapitio na mahakama za nchi hiyo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana