Pata taarifa kuu
MISRI-USALAMA-AJALI

Sissi: Tukio la magari kugongana ni kitendo cha kigaidi

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi amesema kuwa kugongana kwa magari kadhaa mjini Cairo usiku wa leo Jumatatu na kusababisha vifo vya watu 20 ni kitendo cha "kigaidi".

Wachunguzi mbele ya eneo la ajali ya magari yaliyogongana na kusababisha mlipuko mkubwa, Agosti 5, 2019.
Wachunguzi mbele ya eneo la ajali ya magari yaliyogongana na kusababisha mlipuko mkubwa, Agosti 5, 2019. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Rais Sissi, kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa salamu za rambirambi "kwa raia wa Misri na familia za wahanga waliouawa katika tukio hilo ambao chanzo chake ni ugaidi".

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Wizara ya Afya, watu wasiopungua 20 wamefariki dunia wakati gari ndogo iliyokuwa ikiendeshwa kwa kasi kubwa kugonga magari mengine matatu, na kusababisha mlipuko mkubwa usiku wa Jumapili kuamkia leo Jumatatu, muda mfupi tu kabla ya alfajiri.

Wizara ya Mambo ya ndani imelihusisha kundi dogo la Hasm kuwa limehusika na kitendo hicho. Serikali inachukulia kundi hili kama lina ukaribu na kundi la Muslim Brotherhood , kundi lililopigwa marufuku na kuangamizwa nchini Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.