Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA-MKATABA-AMANI

Hatimaye mkataba utakaosaidia uundwaji wa serikali ya mpito Sudan watiwa saini

Wanajeshi na viongozi wa waandamanaji nchini Sudan, hatimaye wametiliana saini mkataba wa kikatiba  utakaowaongoza katika serikali ya mpito, baada ya miezi saba ya mzozo wa kisiasa.

Viongozi wa waandamanaji nchini Sudan Ahmed Rabie akisalimiana na kiongozi wa kijeshi Jenerali Mohamed Hamdan Daglo baada ya kutiliana saini Agosto 4 2019
Viongozi wa waandamanaji nchini Sudan Ahmed Rabie akisalimiana na kiongozi wa kijeshi Jenerali Mohamed Hamdan Daglo baada ya kutiliana saini Agosto 4 2019 AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo unaweka wazi namna taifa hilo litakavyoelekea katika serikali ya kiraia, baada ya serikali ya mpito kumalizika baada ya miaka mitatu.

Kiongozi wa waandamanaji Ahmed Rabie na naibu kiongozi wa baraza la kijeshi Jenerali Mohamed Hamdan Daglo, ndio waliotia saini mkataba huo ulioshuhudiwa na wasuluhishi kutoka nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika.

Aidha, imekubaliwa kuwa kamati maalum iundwe ili kuchunguza mauaji ya mamia ya watu waliopoteza maisha wakati wa maandamano ya kushinikiza kuachia madaraka kwa rais wa zamani Omar Al Bashir.

Wananchi wa Sudan wamekuwa wakisherehekea hatua hii kuelekea utiwaji saini, utakaofanyika mbele ya wananchi wa wageni kutoka nje ya nchi tarehe 17 mwezi huu, siku ambayo rais wa zamani Omar Al Bashir anatarajiwa kupelekwa Mahakamani.

Inatarajiwa kuwa baada ya tarehe 17 wanajeshi na viongozi wa serikali wataunda serikali hiyo ya mpito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.