Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Meya wa Mogadishu afariki dunia Doha, Qatar

media Mwakilishi Maalum mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, James Swan (kushoto), akipokelewa na Meya wa Mogadishu Abdirahman Omar Osman (kulia) muda mfupi kabla ya shambulio dhidi ya ofisi ya Meya, Julai 24, 2019. UNSOM

Meya wa mji wa Mogadishu nchini Somalia, Abdirahman Omar Osman, amefariki dunia baada ya kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa muhanga lililoua watu sita juma lililopita mjini Mogadishu. Amefariki dunia mjini Doha, Qatar, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Abdirahman Omar Osman alijeruhiwa wakati shambulio la kujitoa mhanga katika ofisi yake walipokuwa katika mkutano wa masuala ya usalama.

Abdirahman Omar Osman ambaye aliishi katika mji wa London nchini Uingereza baada ya kuitoroka nchi yake kufuatia kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, alirejea nchini Somalia mwaka 2008 kusaidia kuijenga upya nchi yake inayoendelea kukumbwa na mdororo wa usalama.

Katika ukurasa wa twitter, ujumbe wa Marekani nchini Somalia umemtaja bwana Osman kuwa ''mshirika mzuri sana na aliyekuwa akiwatumikia raia wa Somalia bila kuchoka''.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana