Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mazungumzo kati ya jeshi na viongozi wa maandamano yaahirishwa Sudan

media Wananchi wa Sudan wakisherehekea katika mitaa ya Khartoum tangazo la makubaliano kati ya jeshi na viongozi wa maandamano ili kukomesha mgogoro, Julai 5, 2019. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Mazungumzo yaliyopangwa Ijumaa wiki hii kati viongozi wa maandamano na utawala wa kijeshi nchini Sudan ili kukamilisha pointi ambazo pande zote mbili zimekuwa bado zikitafautiana baada ya kumalizika kwa mkataba wa kugawana madaraka, umeahirishwa, kwa mujibu wa viongozi wa maandamano.

"Mazungumzo yameahirishwa," Omar al-Digeir, mmoja kati ya viongozi wa maandamano, ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Tunahitaji mashauriano zaidi ili kufikia msimamo mmoja," amesema, bila kutaja tarehe mpya ya mazungumzo.

Kiongozi mwingine wa maandamano, Siddig Youssef, pia amethibitisha kuahirishwa kwa mazungumzo hayo.

Jumatano, pande hizo mbili zilifikia "tamko la kisiasa", makubaliano ya kugawana madaraka kati ya Baraza la kijeshi lililochukuwa nafasi ya rais aliyepinduliwa madarakani Omar al-Bashir, mwezi Aprili, na viongozi wa maandamano, hatua ya kwanza kuelekea serikali ya kiraia, madai muhimu ya waandamanaji.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana