Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Jeshi na viongozi wa maandamano watia sahihi tamko la kisiasa la kugawana madaraka Sudan

media Kiongozi nambari mbili wa Baraza la kijeshi Sudan, Mohamed Hamdan Daglo (kulia) pamoja na kiongozi wa maandamano (kushoto) wakitia sahihi tamko la kisiasa la kugawana madaraka katika kipindi cha mpito, mbele ya wasuluhi kutoka Ethiopia na Umoja wa Afrika. © AFP

Wawakilishi wa utawala wa kijeshi na viongozi wa waandamano nchini Sudan wametia sahihi "tamko la kisiasa" la kugawana madaraka katika kipindi cha mpito, baada ya Omar al-Bashir kutimuliwa madarakani mwezi Aprili, waandishi wa habari wa shirika la Habari la AFP wamebaini.

Mazungumzo bado yatafanyika katika siku zijazo kuhusu pointi nyingine zinazoendelea kuzua mgongano kwenye makubaliano yaliyofikiwa Julai 5 kati ya pande mbilii, kulingana na wawilishi wa waandamanaji.

"Tamko la kisiasa" limetiliwa saini na pande mbili baada ya mazungumzo marefu usiku wa Jumanne kuamkia leo Jumatano.

Baada ya mkutano katika hoteli moja ya kifahari jijini Khartoum, kiongozi namba 2 wa Barazala Kijeshi, Mohamed Hamdan Daglo kwa jina maarufu "Hemeidti", pia Mkuu wa kikosi cha kupambana na fujo (RSF), amepongeza hatua hiyo akiita ni ya "kihistoria ".

"Leo tumekubaliana kuhusu tamko la kisiasa," Ibrahim al-Amin, mmoja wa viongozi wa maandamano, ameliambia shirika la Habari la AFP. "Kuhusu nakala ya katiba, tutaanza tena mazungumzo siku ya Ijumaa," amesema.

Mkataba huu ni hatua ya kwanza kuelekea serikali ya kiraia, iliyoombwa na wananchi wengi wa Sudan kwa karibu miezi saba.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana