Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 09/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 09/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 09/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Watu 11 wapatikana wamefariki dunia katika jela la polisi Burkina Faso

media Gari la polisi katika mtaa wa Ouagadougou, Burkina Faso. (Picha ya kumbukumbu) LUDOVIC MARIN / AFP

Watu kumi na mmoja wamepatikana wamekufa katika kituo cha idara ya polisi inayopambana na madawa ya kulevya mjini Ouagadougou, nchini Burkina Faso. Watu hao walikuwa wamezuiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

Mwendesha mashitaka ametangaza kuwa uchunguzi umeanzishwa ili kujua mazingira ya vifo vya watu hao.

Watu hao waliopatikana wamekufa, ni sehemu ya kundi la watu waliokamatwa Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa uchunguzi kuhusu matumizi ya biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.

Watu kadhaa, ikiwa ni pamoja na wateja, wauzaji, wasambazaji na watumiaji, walikamatwa katika idara ya polisi inayopambana na madawa ya kulevya, kulingana na chanzo cha usalama.

Mwendesha mashitaka wa Burkina Faso amefahamisha kwamba uchunguzi umeanzishwa mara moja ili kujua mazingira ya vifo vya watu hao. Wataalamu wa kisayansi wameanza vipimo na kuchunguamiili ya watu hao.

Watuhumiwa kadhaa waliokamatwa katika kesi hiyo wamepelekwa katika vituo vya afya kwa ajili ya vipimo vya ziada ili kujua kama maisha yao hayako hatarini.

"Tunapaswa kujua haraka kama watu hawa hawakumeza kete za madawa ya kulevya au vitu vingine hatari," chanzo cha usalama kimeongeza.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana