Mwendesha mashitaka ametangaza kuwa uchunguzi umeanzishwa ili kujua mazingira ya vifo vya watu hao.
Watu hao waliopatikana wamekufa, ni sehemu ya kundi la watu waliokamatwa Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa uchunguzi kuhusu matumizi ya biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.
Watu kadhaa, ikiwa ni pamoja na wateja, wauzaji, wasambazaji na watumiaji, walikamatwa katika idara ya polisi inayopambana na madawa ya kulevya, kulingana na chanzo cha usalama.
Mwendesha mashitaka wa Burkina Faso amefahamisha kwamba uchunguzi umeanzishwa mara moja ili kujua mazingira ya vifo vya watu hao. Wataalamu wa kisayansi wameanza vipimo na kuchunguamiili ya watu hao.
Watuhumiwa kadhaa waliokamatwa katika kesi hiyo wamepelekwa katika vituo vya afya kwa ajili ya vipimo vya ziada ili kujua kama maisha yao hayako hatarini.
"Tunapaswa kujua haraka kama watu hawa hawakumeza kete za madawa ya kulevya au vitu vingine hatari," chanzo cha usalama kimeongeza.