Pata taarifa kuu
DRC-ICC-NTAGANDA-HAKI

Kesi ya Ntaganda: Upande wa utetezi kukata rufaa

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imemtia hatiani mbabe wa zamani wa kivita wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jenerali Bosco Ntaganda, maarufu kama The Terminator (Mmaliziaji) kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.

Kiongozi wa zamani wa kivita Bosco Ntaganda anaingia mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili, Hague, Septemba 2, 2015.
Kiongozi wa zamani wa kivita Bosco Ntaganda anaingia mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili, Hague, Septemba 2, 2015. AFP PHOTO/ POOL / MICHAEL KOOREN
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ICC Bosco Ntaganda alihusika kwa kiasi kikubwa katika machafuko yaliyotokea mwaka 2002 na 2003 katika Jimbo la Ituri.

"Bw Ntaganda, kwa sababu nilizoelezea, Mahakama, baada ya kusikia ushahidi wote uliotolewa na pande mbalimbali, ninakuhukumu kwa mauaji ambayo ni" uhalifu dhidi ya binadamu ". Neno "hatia" lilisomwa mara 18 katika chumba cha mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, huku Bosco Ntaganda akiinamisha kichwa chake chini.

Hata hivyo upande wa utetezi umesema unajiandaa kukata rufaa.

Kwa mujibu wa mmoja wa wanasheria wake wakili Stephane Bourgon, Bosco Ntaganda, raia wa DRC, mwenye asili ya Rwanda amefanyiwa unyonge na amebaini kwamba ana nia ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu.

Majaji wa mahakama wamemtia hatiani Ntaganda kwa makosa 13 ya uhalifu wa kivita na matano ya uhalifu dhidi ya binadamu, kwa ajili ya jukumu lake kwenye mgogoro wa kikatili wa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali na vyama vya kiraia vimekaribisha uamuzi huo wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

Awali Bosco Ntaganda alithibitisha Mahakama kwamba alikuwa alilinda raia katika vita vyake katiak Jimbo la Ituri, huku akijipongeza jinsi alivyoendesha vita katika eneo hilo kwa kwa kipindi cha miaka 17.

Hukumu dhidi yake inatarajiwa kutolewa katika wiki zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.