Pata taarifa kuu
DRC-ICC-NTAGANDA-HAKI

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu yamtia hatiani Bosco Ntaganda

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imemtia hatiani kiongozi wa zamani wa kivita nchini DRC Bosco Ntaganda. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imemtia hatiani kwa uhalifu wa kvita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Kiongozi wa wanamgambo DRC Bosco Ntaganda, Septemba 2, 2015, wakati wa ufunguzi wa kesi yake mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Hague.
Kiongozi wa wanamgambo DRC Bosco Ntaganda, Septemba 2, 2015, wakati wa ufunguzi wa kesi yake mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Hague. © REUTERS/Michael Kooren
Matangazo ya kibiashara

Mbabe huyo wa zamani wa kivita, mwenye umri wa miaka 45, alihusika katika machafuko yalityotekelezwa mnamo mwaka 2002 na 2003 katika Jimbo la Ituri, kaskazini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ntaganda atasimama mbele ya majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita, ICC, kujibu mashtaka ya tuhuma za kusimamia mauji na kuwatumia watoto kwenye jeshi lake la waasi.

Ntaganda anakabiliwa na makosa 13 ya uhalifu wa kivita na matano ya uhalifu dhidi ya binadamu, kwa ajili ya jukumu lake kwenye mgogoro wa kikatili wa vita ya wenyewe kwa wenyewe katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Ntaganda ambaye ana asili ya Rwanda, mnamo mwezi Septemba 2015 alikanusha kuhusika na uhalifu huo mwanzoni mwa kesi yake mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.

Waendesha mashitaka katika mahakama ya ICC iliyoko mjini the Hague, wanasema jeshi lake la waasi kati ya mwaka 2002 na 2003 lilifanya utawala wa hofu katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Ituri, na kusababisha unyanyasaji wa kutisha dhidi ya wenyeji.

Ntaganda alipanga operesheni za jeshi lake la Patriotic Forces for the Liberation of Congo (FPLC), akiwatumia watoto kama askari na kuwalazimisha wanawake katika utumwa wa ngono, wakati akiwashambulia raia kwa misingi ya kikabila.

Mahakama ya ICC imesema hukumu dhidi ya kongozi huyo wa zamani wa waasi itatolewa leo Jumatau Julai 8.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.