Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAZUNGUMZO-SIASA

Kaimu rais wa Algeria aitisha mazungumzo ya kitaifa

Kaimu rais wa Algeria Abdelkader Bensalah ametoa wito kwa "mazungumzo ya kitaifa yatakayowashirikisha wadau wote" ili kuandaa uchaguzi wa urais. Hata hivyo jeshi na serikali hawatashirikishwa katika mazungumzo hayo.

Kaimu rais wa Algeria Abdelkader Bensalah akihutubia taifa kwenye televisheni ya taifa, tarehe 3 Julai 2019.
Kaimu rais wa Algeria Abdelkader Bensalah akihutubia taifa kwenye televisheni ya taifa, tarehe 3 Julai 2019. Algerian TV / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kaimu rais wa Algeria amelihutubia taifa Jumatano hii, Julai 3, hotuba ambayo imerushwa moja kwa moja kwenye runinga ya taifa. Abdelkader Bensalah amehakikisha kwamba serikali wala jeshi hawahusiki katika mazungumzo hayo.

Mazungumzo hayo yatafanyika "kwa uhuru na uwazi," ameahidi Abdelkader Bensalah. Yatataongozwa na "watu raia wa Algeria wenye sifa za kuaminika, watu walio huru, ambao hawana upande wowote wanaoegemea".

Serikali wala jeshi hawatashiriki katika mazungumzo hayo. Serikali itawajibika tu na "kukamilisha uwezo wote kwa jopo la watu watakaoongoza mazungumzo hayo".

"Majadiliano haya ni ya dharura" na "muhimu", amesema Kaimu rais waAlgeria'. Mazungumzo haya [...] yatazingatia lengo moja tu la kimkakati la kuandaa uchaguzi."Uchaguzi ambao "utafanyika haraka iwezekanavyo".

Kuwekwa kwa "chombo" au "mamlaka huru" ya "kuandaa na kudhibiti mchakato wa uchaguzi katika hatua zake zote" itakuwa "katika agenda ya mazungumzo".

Uchaguzi wa urais ulikuwa umepangwa kufanyika Alhamisi hii, Julai 4. Lakini kutokana na kukosekana kwa wagombea, uchaguzi huo haukuweza kufanyika. Abdelkader Bensalah anatakiwa kusalia madarakani hadi uchaguzi wa rais mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.