Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Kambi ya jeshi yakabiliwa na mashambulizi makubwa magharibi mwa Niger

media Des soldats nigériens patrouillent dans la région d'Ayorou, au nord-ouest … Askari wa Niger wakipiga doria katika eneo la Ayorou, kaskazini-magharibi mwa Niamey, Niger (picha ya kumbukumbu). © ISSOUF SANOGO / AFP

Kundi la watu wa kujitoa muhanga waliendesha mashambulizi makubwa katika kambi ya jeshi ya Eneo la Inates magharibi mwa Niger, karibu na mpaka na Mali. Hali ya usalama nchi Niger bado ni tete.

Duru za kuaminika, zinaeleza kwamba mashambulizi hayo yalitekelezwa kwa kutumia "magari yaliyotegwa mabomu".

Kwa mujibu wa mashahidi kundi la wauaji wasiojulikana waliokuwa kwenye magari na pikipiki waliendesha mashambulizi ya kigaidi katika kambi ya jeshi katika eneo la Inates Jumatatu mchana.

Mashambulizi makubwa yametekelezwa na magari mawili yaliyotegwa magomu ambayo yalilipuka katikati ya kambi ya jeshi. wakati huo huo kundi la wanajihadi walio kuwa kwenye pikipiki walirusha risasi na kuzingira kituo cha askari.

Kulingana na vyanzo kadhaa vya usalama, mapigano makali yameripotiwa.

Hata hivyo hakuna idadi rasmi ya watu waliopoteza maisha katika mapigano hayo lakini inaelezwa tu kwamba kambi zote mbili (waasi na jeshi) wamepoteza idadi kubwa ya wapiganaji wao.

Milipuko mikubwa ya magari mawili yaliyosheheni vilipuzi pia imesababisha vifaa kadhaa kuteketea kwa moto ndani ya kambi.

Hata hivyo ndege za kivita za Ufaransa na Marekani zilionekana zikizunguka angani kwenye eneo la tukio kabla ya tukio hilo kutokea. Operesheni ya jeshi ya kuwasaka wauaji hao inaendelea, chanzo cha usalama kilibaini Jumatatu usiku.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana