Pata taarifa kuu
TUNISIA-USALAMA

Hofu yaendelea kutanda Tunis baada ya milipuko miwili

Waziri mkuu wa Tunisia, Youssef Chahed amekashifu mashambulizi mawili ya bomu yaliyotekelezwa mjini Tunis, akiyataja mashambulizi hayo kama ya kutengeneza hofu kwa wananchi.

Gari lililoharibiwa na risasi na kuchomwa moto katikati mwa Tunis, Juni 27, 2019.
Gari lililoharibiwa na risasi na kuchomwa moto katikati mwa Tunis, Juni 27, 2019. Fethi Belaid / AFP
Matangazo ya kibiashara

Matamshi yake yamekuja wakati huu kundi la Islamic State likijinasibu kuhusika na mashambulizi mawili tofauti yaliyosababisha kifo cha askari na kuwajeruhi raia kadhaa.

Habib ni mfanyakazi wa Benki ambae alikuwa karibu na moja miongoni mwa mashambulio hayo ambayo amesema yanatokea ikiwa imesalia miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge.

Hayo yanajiri wakati rais wa nchi hiyo, Beji Caid Essebsi, amelazwa Hospitalini, baada ya kuugua.

Maafisa nchini humo wanasema Essebsi mwenye umri wa miaka 92, na rais mzee zaidi duniani, alilazwa hospitalini wiki iliyopita.

Waziri Mkuu Youssef Chahed amesema serikali inafanya kila inachowezesha kumpa huduma ya hali ya juu kwa rais huyo.

Haijafahamika ni ugonjwa gani unamsumbua rais huyo na serikali imelazimika kutoa taarifa hiyo baada ya uvumi kuwa rais huyo alikuwa amefariki dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.