Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-HAKI

DRC: Waranti wa kukamatwa watolewa dhidi ya Kiongozi wa kivita Guidon

Mahakama ya kijeshi ya mkoa wa Kivu Kaskazini imetoa waranti wa kukamatwa dhidi ya Guidon Shimiray Mwissa, kiongozi wa kivita anaye shtumiwa kutekeleza uhalifu mbalimbali katika eneo hilo.

Guidon Shimiray Mwissa anashtumiwa na vyanzo kadhaa katika ongezeko la uhalifu huko Masisi, Kivu Kaskazini.
Guidon Shimiray Mwissa anashtumiwa na vyanzo kadhaa katika ongezeko la uhalifu huko Masisi, Kivu Kaskazini. ALEXIS HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

RFI imeweza kupata hati iliyotolewa tarehe 7 Juni 2019, ambayo Mwendesha mashitaka wa kijeshi, Jenerali Timothée Mukuntu, ameithibitisha.

"Guidon Shiniray Mwissa anakabiliwa na mashitaka ya kushiriki katika kundi la waasi", "uhalifu wa kivita kwa kuwasajili watoto katika kundi lake" na "uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa ubakaji". Haya ni mashitaka yaliyomo kwenye waranti huo uliotolewa dhidi ya Guidon Shimiray Mwissa na mahakama ya kijeshi, ambayo ilifunguliwa kesi dhidi yake mnamo mwezi Machi 2018. Tangu wakati huo, waathirika kadhaa wamesikilizwa, amesema Mwendesha mashitaka wa kijeshi, Jenerali Timothy Mukuntu.

Guidon Shiniray Mwissa ambaye Tayari anakabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa, anaongoza muungano wa makundi ya waasi wa NDC-R (Nduma Defense of Congo-Renove) tangu mwaka 2015. Kundi ambalo linaendesha vita dhidi ya makundi ya wapiganaji wa Kihutu kutoka nje na yale yanayoundwa na baadhi ya raia wa DRC katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Katika miezi ya hivi karibuni, kwa mujibu wa vyanzo vya Umoja wa Mataifa, Guidon Shimiray Mwissa alipanua eneo lake la kivita kwa kiasi kikubwa, na hatimaye kudhibiti "miji na maeneo ya uchimbaji madini ya Walikale," lakini pia maeneo ya Lubero, Masisi na Rutshuru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.