Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mauritania: Mgombea wa chama tawala atangazwa mshindi, upinzani wapinga matokeo

media Mgombea wa chama tawala Mohamed ould Ghazouani (katikati), wakati wa akipiga kura, Nouakchott, Juni 22, 2019.Bw Ghazouani amechaguliwa kwa kura ya 52%, kulingana na matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na CENI Jumapili jioni Juni 23. © SIA KAMBOU / AFP

Mgombea wa chama tawala nchini Mauritania, Mohamed Ould Ghazouani ameshinda kiti cha urais kwa asilimia 52 ya kura katika uchaguzi wa mwishoni mwa juma.

Tayari kiongozi wa upinzani nchini humo Biram Ould Dah Ould Abeid aliyepata asilimia 18.58 ya kura amekataa kutambua matokeo hayo akilalamika kuwepo kwa udanganyifu.

Kwa upande wao chama tawala kupitia mshauri wa masuala ya kisiasa wa rais mteule, Mohamed Salem Ould Merzoug anasema upinzani unayo njia moja tu nayo ni kwenda mahakamani kupinga ushindi wao.

Uchaguzi huu utaonesha zoezi la kwanza la kukabidhiana madaraka kati ya marais wawili waliochaguliwa katika nchi hii kubwa ya kanda ya Sahel iliyokumbwa na mapinduzi mbalimbali ya kijeshi tangu mwaka 1978 hadi mwaka 2008, tarehe ya mapinduzi yaliyomwezesha Mohamed Ould Abdel Aziz kuingia madarakani, kabla ya kuchaguliwa kwake mwaka 2009. Kulingana na katiba ya nchi hiyoMohamed Ould Abdel Aziz hangeweza kuwania tena baada ya mihula yake miwili.

Bw Ghazouani alijitangaza mshindi kufuatia matokeo ya uchaguzi kutoka 80% ya vituo vya kupigia kura, baada ya kumalizika zoezi la kupiga kura usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili mbele ya rais anaye maliza muda wake Ould Abdel Aziz.

Upinzani umelichukulia tangazo hilo kama "jaribio jipya la mapinduzi" linaloendeshwa na Majenerali wawili wa zamani.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana