Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MACHAFUKO-USALAMA

Jenerali anayechukuliwa kama muhusika mkuu wa mashambulizi nchini Ethiopia auawa

Mkuu wa usalama katika Jimbo la Amhara, Jenerali Asaminew Tsige, ambaye anachukuliwa kama muhusika mkuu wa mashambulizi mawili siku ya Jumamosi, ameuawa Jumatatu wiki hii, kwa mujibu wa televisheni ya EBC, ilio karibu na utawala.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alionekana kwenye televisheni ya serikali akivalia sare ya jeshi Jumamosi usiku , akitangaza kufanyika kwa jaribio la mapinduzi Dahir Bar.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alionekana kwenye televisheni ya serikali akivalia sare ya jeshi Jumamosi usiku , akitangaza kufanyika kwa jaribio la mapinduzi Dahir Bar. HO / Ethiopian TV / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yaliyogharimu maisha ya Mkuu wa jeshi ya nchi hiyo na maafisa kadhaa waandamizi katika jimbo la Amhara.

Kituo cha televisheni cha EBC kimebaini katika katika muhtasari wa habari kwamba Jenerali Asaminew, "ambaye alikuwa mafichoni tangu jaribio la mapinduzi lililotibuliwa mwishoni mwa wiki hii iliyopita, alipigwa risasi katika eneo la Zenzelma huko Bahir Dar" , mji wa kaskazini magharibi mwa Ethiopia.

Jenerali Saare na Gavana wa Amhara, bwana Ambachew Mekonnen ambaye pia aliuawa Jumamosi, walikuwa wakionekana kama washirika wakubwa wa Waziri Mkuu Abiy.

Bendera zinapepea nusu mlingoti baada ya serikali kutangaza kuwa siku ya maombolezo.

Brigedia Jenerali Asaminew Tsige, ambaye alikuwa ni miongoni mwa maafisa wa juu wa jeshi walioachiwa huru mwanzoni mwa mwaka jana baada ya serikali iliyopita kuwaachia wafungwa wa kisiasa kutokana na msukumo kutoka kwa umma, alikuwa ni mkuu wa usalama wa jimbo la Amhara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.