Naibu mwenyekiti wa CENI nchini DRC ajiuzulu
Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo CENI, Norbert Basengezi ametangaza kujiuzulu wadhifa wake.
Imechapishwa:
Basengezi amechukua hatua hiyo wakati huu anapoendelea kukabiliwa na vikwazo kutoka kwa Marekani.
Marekani ilichukua hatua hiyo baada ya kuchelewesha matokeo ya Uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Desemba mwaka 2018.
Taarifa kutoka Tume ya Uchaguzi CENI, imesema kuwa Basengezi amewasilisha barua kwa rais Felix Tshisekedi.
Hata hivyo, ni lazima rais Tshisekedi akubali kujiuzulu kwake.
Aliyekuwa mgombea wa upinzani Martin Fayulu ameendelea kuishtumu Tume ya Uchaguzi kwa kumuibia kura na kumpa ushindi Tshisekedi.