Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-WABUNGE-MASENETA

MCL: Mahakama ya Katiba nchini DRC kusikiliza malalamishi ya wapinzani

Mahakama ya Katiba nchini DRC imesema itapitia upya, uamuzi wake wa awali wa kufuta kuchaguliwa kwa wabunge 30 wa upinzani na nafasi hizo kukabidhiwa kwa muungano wa kisiasa wa FFC, unaongozwa na rais wa zamani Joseph Kabila.

Mahakama ya Katiba jijini Kinshasa nchini DRC
Mahakama ya Katiba jijini Kinshasa nchini DRC © RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Chama cha upinzani cha MLC kikiongozwa na Naibu Mwenyekiti Jacques Ndjoli amesema kuwa rais wa Mahakama hiyo ameahidi kusikiliza malalamishi ya wapinzani.

Ndjoli ameongeza kuwa hatua imekuja baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Mahakama hiyo jijini Kinshasa.

"Rais wa Mahakama ya Katiba amesema, uamuzi unafanywa na binadamu huenda makosa yakatokea na kwa sababu ya hili, huenda sheria ilitafsiriwa visivyo," amesema.

Baada ya uamuzi huo uliowashangaza wengine, vuguvugu la upinzani la Lamuka, limeapa kususia vikao vyote vya bunge na Senate hadi pale nyadhifa hizo zitakaporejeshwa kwa wapinzani waliokuwa wameshinda viti hivyo.

Wiki hii, mgombea wa urais kupitia Lamuka mwaka 2018 Martin Fayulu alinukuliwa akishtumu uamuzi huo wa Mahakama na kusema, inaonesha namna gani rais wa zamani Kabila, anaendelea kuongoza nchi hiyo kwa njia ya mgongo.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.