Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-KASAI-KAMWINA-NSAPU

UN yaitaka DRC kuwachukulia hatua waliowauwa mamia ya watu mkoani Kasai

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokraisa ya Congo kuongeza kasi na juhudi kuhakikisha kuwa watu waliohusika na vitendo vya kihalifu kwenye mkoa wa  Kasai wanawajibishwa.

Mtoto katika mkoa wa Kasai
Mtoto katika mkoa wa Kasai AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yao mpya, wataalamu hao wameonya kuwa utawala wa Kinshasa unafanya kazi taratibu kuchunguza na kuwashtaki mamia ya watuhumiwa wa vitendo vya kihalifu na dhulma dhidi ya binadamu vilivyotekelezwa  kati ya mwaka 2016 na 2017.

Ripoti iznasema kuwa katika kipindi cha miaka 3 iliyopita, ni kesi moja tu ndio ambayo iko tayari kusikilizwa, suala ambalo ambalo halitoa matumaini ya washukiwa kushtakiwa.

Aidha, ripoti ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa watu 500 waliuawa katika mkoa wa Kasai, yanayoaminiwa kutekelezwa na waasi wa Kamwina Nsapu.

Machafuko huko Kasai yamesababisha watu karibu Milioni 1.3 kuyakimbia makwao, takwimu zikionesha kuwa 8,000 wanakimbia kila siku na wengine kwenda nchi jirani ya Angola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.