Pata taarifa kuu
SUDAN-UN-AMANI-USALAMA-CHINA-URUSI

China na Urusi zazuia azimio kulaani mauaji nchini Sudan

Nchi ya China ikiungwa mkono na Urusi, zimezuia kupitishwa kwa azimio katika  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,  kulaani mauaji ya raia nchini Sudan wakati Jumuiya ya kimataifa ikiwekewa shinikizo kukomesha machafuko yanayoendelea.

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura.
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura. UN Photo/Loey Felipe
Matangazo ya kibiashara

Katika kikao cha faragha cha baraza hilo, Uingereza na Ujerumani zilikuwa zimesambaza taarifa kwa wanahabari wakitoa wito kwa watawala wa kijeshi na waandamanaji kuendelea kuzungumza ili kupata suluhu ya pamoja.

Hata hivyo, China ilikataa pendekezo hilo huku Urusi ikisisitiza baraza hilo kusubiri kwanza majibu kutoka Umoja wa Afrika ambao umekuwa ukishiriki tangu awali kujaribu kutuliza mzozo wa Sudan.

Baraza la amani na Usalama la Umoja wa Afrika, linakutana siku ya Jumatano kujadili hali inayoendelea kushuhudiwa nchini Sudan, wakati huu uongizi wa kijeshi ukiomba radhi baada ya wanajeshi kutumia nguvu na kuahidi kuchunguza kilichotokea.

Madaktari nchini Sudan wanasema kuwa watu 60 walipoteza maisha baada ya kupigwa risasi na maafisa wa usalama.

Naibu balozi wa Urusi kwenye umoja wa Mataifa Dmitry Polyanskiy, amenukuliwa akisema pendekezo lililowasilishwa halikuwa na usawa na kuzitaka nchi nyingine wanachama kuwa makini na hali inayojiri Sudan.

Baada ya pendekezo hilo kukataliwa, nchi 8 za Ulaya zilitoa taarifa ya pamoja kulaani mashambulizi dhidi ya raia yaliyotekelezwa na vyombo vya usalama vya Sudan.

Ubelgiji, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Poland, Sweden na Uholanzi zimesema uamuzi wa baraza la kijeshi kusitisha makubaliano ya awali pamoja na kuendelea na mazungumzo huku likitoa muda mfupi wa kufanya uchaguzi suala ambalo viongozi wa waandamanaji wamekataa na kuitisha maandamano zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.