Pata taarifa kuu
WAISLAMU-EID-SHEREHE-DINI

Waislamu duniani waanza kuadhimisha sikukuu ya Eid al-Fitr

Baadhi ya Waislamu katika mataifa mbalimbali ya bara Afrika kama Uganda, Ethiopia, Burundi na DRC wanaadhimisha siku ya Eid al-Fitr  siku ya Jumanne, baada ya Mali kuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo siku ya Jumatatu.

Waislamu mjini Jerusalem nchini Israel
Waislamu mjini Jerusalem nchini Israel middleeastmonitor.com
Matangazo ya kibiashara

Aidha, Waislamu katika mataifa ya Ghuba kama vile Qatar, kuwait na Fale za Kiarabu pia wanaadhimisha Eid al-Fitr siku ya Jumanne,

Hata hivyo, idadi kubwa ya Waislamu wataadhimsha siku hii muhimu katika kalenda ya dini hiyo siku ya Jumatano kwa sababu ya kuandama kwa mwezi.

Siku ya Eid, huadhimishwa na Waislamu wote duniani, baada ya kumaliza mfungo wa siku 30, unaofahamika kama mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Idadi kubwa ya Waislamu nchini Tanzania na Kenya wanatarajiwa kuadhimisha Eid al-Fitr siku ya Jumatano.

Eid al-Fitr  ni siku ya mapumziko katika mataifa mengi duniani.

Kuna Waislamu zaidi ya Bilioni 1.8 duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.