Pata taarifa kuu
SUDAN

Jeshi lawaonya waandamanaji, lafunga ofisi za kituo cha Aljazeera

Watawala wa kijeshi nchini Sudan wanasema kuwa kambi za waandamanaji mjini Khartoum zimekuwa tishio kwa usalama wa taifa, wakati huu jeshi likiagiza kufungwa kwa ofisi za kituo cha habari cha Aljazeera.

Waandamanaji wa Sudan wakiwa na mabango katika moja ya maandamano yao ya hivi karibuni.
Waandamanaji wa Sudan wakiwa na mabango katika moja ya maandamano yao ya hivi karibuni. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa waliyoitoa kupitia televisheni ya taifa, msemaji wa baraza la kijeshi amesema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu aliosema waharibifu.

Kwa miezi kadhaa sasa waandamanaji wameendelea kutia ngumu kutoka kwenye maeneo yanayozingira makao makuu ya jeshi wakishinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

"Eneo la maandamano limekuwa si salama na linahatarisha usalama wa taifa," alisema Jenerali Bahar Ahmed Bahar, mkuu wa jeshi mjini Khartoum.

Jeshi linasema magari maalumu ya kijeshi ya kikosi maalumu yamekuwa yakishambuliwa na mengine kuzuiliwa na waandamanaji kwenye eneo la maandamano.

Eneo hilo limekuwa kitovu cha vuguvugu la maandamano, ambayo yalishuhudia kuondoka madarakabi kwa rais Omar al-Bashir aliyeondolewa na jeshi mwezi uliopita, na tangu wakati huo wamekuwa wakitaka wanajeshi nao kukabidhi madaraka kwa raia.

Mashambulizi dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari.

Katika hatua nyingine, mamlaka nchini humo zimekipa taarifa kituo cha habari cha Aljazeera kufunga ofisi zake mjini Khartoum kwa maelekezo ya baraza la kijeshi, bila hata ya kutoa sababu.

Uamuzi huu wa jeshi unamaanisha pia kunyang'anywa vibali vya kufanyia kazi nchini humo kwa wawakilishi wa kituo hicho pamoja na wafanyakazi wengine.

Katika taarifa yake uongozi wa Aljazeera umekashifu hatua ya baraza la kijeshi, wakisema kitendo hiki ni ukiukaji mkubwa wa uhuru wa watu kutoa na kupata habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.