Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Sudan: Upinzani wagawanyika kuhusu maandamano mapya

media Waandamanaji wakiwa nje ya makao makuu ya Jeshi nchini Sudan. Photo: Ashraf Shazly/AFP

Chama kikuu cha upinzani nchini Sudan pamoja na baadhi ya viongozi wa waandamanaji wamekataa wito wa kushiriki maandamano ya siku mbili yanayotarajiwa kufanyika Jumanne na Jumatano ya wiki hii kushinikiza jeshi kukabishi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Msimamo huu wa upinzani ni ishara za kugawanyika ndani ya vuguvugu la mabadiliko linaloshiriki mazungumzo na baraza la kijeshi.

Mazungumzo kati ya viongozi walioko chini ya mwavuli wa maandamano, the Alliance for Freedom and Change pamoja na majenerali wa jeshi ambao wanaongoza nchi hiyo baada ya kumuondoa madarakani Omar al-Bashir mwezi uliopita, yamekuwa yakisuasua pande zote zikivutana kuhusu nani aongoze Serikali ya mpito.

Katika jitihada zao za kuweka shinikizo kwa baraza la kijeshi linalitawala, viongozi wa waandamanaji waliitisha maandamano ya nchi nzima kuanzia Jumanne ya wiki hii, lakini chama cha Umma, ambacho ndio muhimili wa upinzani kimekataa wito wa kuandamana.

Taarifa ya chama cha Umma imesema “tunakataa maandamano yaliyotangazwana baadhi ya makundi ya upinzani, mgomo wa kitaifa ni silaha ambayo inapaswa kutumika baada ya kukubaliwa na kila upande,” imesema taarifa hiyo.

“Tunapaswa kuepuka njia za namna hii ambazo zinaweza kuharibu mambo na ambazo hazijakubaliwa.”

Chama cha Umma ambacho kinaongozwa na waziri mkuu wa zamani Sadiq al-Mahdi, kimesema uamuzi wa kuitisha mgomo wa nchi nzima unapaswa kuchukuliwa na baraza la viongozi wa maandamano.

Baraza la namna hii bado halijaundwa “na litaundwa katika kikao cha juma hili.” imeongeza taarifa ya chama hicho.

Ilikuwa ni serikali ya waziri mkuu Mahdi yenyewe ambayo Bashir aliyeondolewa April 11. iliipindua iliyokuwa serikali ya kiislamu mwaka 1989.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na shirika la habari la AFP, Mahdi amewaonya waandamanaji wasiwachokoze wanajeshi wanaotawala, ambaop kwa sehemu kubwa amesema walikuwa sehemu ya kumuondoa madarakani Bashir.

Katika hatua nyingine, wakati huu ambapo mazungumzo kati ya viongozi wa waandamanaji na wanajeshi yakiahirishwa, vuguvugu la kiislamu linalounga mkono jeshi, lina imani kuwa watawala hao wataendeleza utawala wa sharia uliopo.

Vyama vya kiislamu ambavyo vyenyewe vimekuwa nje tangu kuanza kwa maandamano ya kumuondoa madarakani rais Bashir, bado havijatangaza kuungana na vyama vingine katika mazungumzo yanauoendelea kupata serikali ya kiraia ambayo kwa makubaliano yaliyopo, itaongoza kwa miaka mitatu.

Hivi karibu wafuasi wa vyama hivyo waliandamana kwenye mji mkuu Khartoum kueleza kuwa hawataunga mkono makubaliano yoyote ambayo yatapelekea kufutwa kwa utawala wa sharia nchini humo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana