Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-SIASA-LAMUKA

DRC: Katumbi arejea nyumbani na kupokelewa na maelfu mjini Lubumbashi

Mwanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Moise Katumbi Chapwe, amerejea nyumbani mjini Lubumbashi, na kupokelewa na maelfu ya wafuasi wake.

Kesi ya mwanasiasa wa upinzani DRC, Moise Katumbi, ambaye yuko uhamishoni, imesikilizwa Jumatano huko Kinshasa.
Kesi ya mwanasiasa wa upinzani DRC, Moise Katumbi, ambaye yuko uhamishoni, imesikilizwa Jumatano huko Kinshasa. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Katumbi amekuwa akiishi nje ya nchi hiyo kwa karibu miaka mitatu, baada ya kukimbilia nje ya nchi kwa sababu ya tofauti za kisiasa na rais wa zamani Joseph Kabila.

Akiwa jijini Brussels nchini Ubelgiji alikokuwa anaishi, Katumbi alifunguliwa mashtaka ya kuuza nyumba ya mtu binafsi na akahukumiwa jela miaka mitatu, lakini baadaye mashataka hayo yakafutwa.

Mwaka 2018, alijaribu kurejea nyumbani kuwania urais lakini akazuiwa na maafisa wa usalama alipofika katika mpaka wa Kasumbalesha, upande wa Zambia.

Moise Katumbi akiwa ndani ya ndege akirejea nyumbani Mei 20 2019
Moise Katumbi akiwa ndani ya ndege akirejea nyumbani Mei 20 2019 twitter.com/moise_katumbi

Gavana huyo wa zamani wa Katanga, ambaye alitaka kuwa rais, amesema amerudi nyumbani na ujumbe wa amani kwa wananchi wa DRC ili kuendeleza siasa za mabadiliko katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

Kabla ya kuondoka nchini DRC na kwenda upinzani, Katumbi alikuwa mshirika wa karibu wa rais wa zamani Kabila lakini wakatofauatiana kisiasa. Kabila aliwahi kumwita Judas, akiwa anamaana kuwa Katumbi alimsaliti.

Wadadidi wa siasa za DRC wanasema kurejea kwa Katumbi, kunaashiria utulivu wa kisiasa nchini humo chini ya rais Tshisekedi, kiongozi ambaye amesema yeye ni mpinzani wa rais huyo.

Viongozi wa Lamuka walipokutana mwezi April mwaka 2019 jijini Brussels nchini Ubelgiji
Viongozi wa Lamuka walipokutana mwezi April mwaka 2019 jijini Brussels nchini Ubelgiji twitter.com/moise_katumbi

Nini hatima ya Lamuka ?

Kurejea kwa Katumbi, kumefufua matumaini ya kuendelea kwa harakati za kisiasa za vuguvugu la Lamuka, lililowaleta wanasiasa wa upinzani pamoja kumpata mgombea mmoja kupambana na chama tawala wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018.

Mwezi Aprili mwaka 2019, viongozi sita wa Lamuka wakiongozwa na Katumbi walikutana jijini Brussels nchini Ubelgiji na kukubaliana kuwa, Lamuka sasa litakuwa vuguvugu la kisiasa.

Mbali na Katumbi, vuguvugu hilo linaundwa na Jean-Pierre Bemba na Mbusa Nyamwisi, ambao wote bado wanaishi nje ya nchi hiyo.

Mgombea urais wa Lamuka mwaka 2018, Martin Fayulu ameendelea na ziara ya ndani ya nje ya nchi hiyo kuendelea kuonesha kuwa hakubaliana na ushindi wa rais Felix Tshisekedi.

Kabla ya Thisekedi kuhamia katika muungano wa CACH pamoja na Vital Kamehre, wote walikuwa pamoja katika vuguvuvu la Lamuka, kumtafuta mgombea mmoja, baada ya Fayulu kupewa nafasi hiyo, alipata shinikizo, na kuamua kuachana na Lamuka.

Jean-Pierre Bemba na Mbusa Nyamwisi, nao wamesema kuwa wako tayari kurejea nyumbani ili kuendeleza harakati za Lamuka, lakini hawahjasema ni lini watarudi nyumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.