Pata taarifa kuu
LIBYA-SILAHA-VITA-UN

Jeshi nchini Libya lajigamba kuwa na silaha mpya licha ya vikwazo

Jeshi la serikali ya Libya linayotambuliwa kimataifa linasema limepata silaha mpya kuendelea kupambana na vikosi vya upinzani vinavyongozwa na Jenrali Khalifa Haftar.

Silaha za kivita nchini Libya
Silaha za kivita nchini Libya Mahmud TURKIA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwezi Aprili, makabiliano makali yameshuhudiwa kati ya vikosi hivyo pinzani, wakati huu vile vya Haftar anayeongoza eneo la mashariki wa nchi hiyo, vikitaka kudhibiti jiji kuu Tripoli.

Wanajeshi wa serikali ya Libya wanaoungwa mkono na jumuiya ya Kimataifa wamepata silaha mpya licha ya nchi hiyo kuwekewa vikwazo vya kununua silaha, suala ambalo limezua maswali ni wapi walikozitoa.

Serikali jijini Tripoli inasema silaha hizo zimeingia nchini kwa maandalizi ya kufanikisha operesheni dhidi ya waasi wanaongozwa na Haftar.

Picha za magari ya kijeshi zimeonekana katika bandari ya Tripoli lakini pia kwenye ukurasa wa facebook kuthibitisha kuwa silaha hizo zilikuwa zimetoka nje ya nchi hiyo.

Msemaji wa serikai amethibitisha kuwasili kwa silaha hizo lakini hakusema zimetokea wapi.

Tangu mwaka 2011, baada ya kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Moamer Kadhafi na Umoja wa Mataifa kutangaza vikwazo vya kutonunua silaha, makundi mbalimbali yamekuwa yakikiuka masharti hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.