Pata taarifa kuu
DRC-AJALI-USALAMA

Usafiri na usalama wa majini vyaendelea kuzua hofu DRC

Watu saba wameokolewa katika ajali ya mtumbwi iliotokea Jumapili Mei 12 katika Ziwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hakuna aliepoteza maisha katika tukio hilo lililotokea eneo la Muhimba Ruhunde tarafa ya Kalehe.

Ajali za majini zimekuwa sugu katika Ziwa Kivu, mashariki mwa DRC.
Ajali za majini zimekuwa sugu katika Ziwa Kivu, mashariki mwa DRC. Photo MONUSCO/Force
Matangazo ya kibiashara

Mtumbiwi huo ulikuwa umebeba mifuko ya mkaa. Mei 6, watu 2 walipoteza maisha katika ajali kama hiyo huku wengine wakitokomea kusikojulikana. Kupakia mizigo kupita kiasi pamoja na hali ya hewa kuwa mbaya ndio imekuwa chanzo kikuu cha ajali hiyo.

Hii ni ajali ya 6 kutokea katika ziwa Kivu tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2019. Delphin Mbirimbi, mwenyekiti wa mashirika ya kiraia katika tarafa ya Kalehe amesema wananchi hawataki kuachana na tabia ya kutumia mitumbwi iliopakia kupita kiasi.

Watu zaidi ya mia moja na arobaini walipoteza maisha katika ajali kama hiyo iliotokea April 15 katika ziwa Kivu, ambapo rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Thisekedi, ambae alikuwa ziarani katika eneo hilo aliahidi kujenga barabara itokayo Goma kuelekea Kalehe-Bukavu, pamoja na ujenzi wa Bandari kubwa ili kuruhusu meli kubwa kubwa kuegesha katika maeneo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.