Pata taarifa kuu
DRC-ICC-BEMBA-HAKI

Jean-Pierre Bemba aomba ICC euro milioni 68 kama fidia

Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC Jean-Pierre Bemba anaiomba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kulipwa zaidi ya euro milioni 68 kama fidia kutokana na kufungwa bila hatia.

Jean-Pierre Bemba katika mkutano na waandishi wa habari, Brussels Julai 24, 2018.
Jean-Pierre Bemba katika mkutano na waandishi wa habari, Brussels Julai 24, 2018. © REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Jean-Pierre Bemba alishtumiwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliotekelezwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2002 na 2003, lakini aliachiliwa huru mwezi Juni 2018, baada ya kumaliza miaka kumi jela.

Baada ya kukamatwa kwake, Mahakama hiyo ilikamata mali zake, ikiwa ni pamoja na zile za nchini Ureno, Ubelgiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Makamu wa rais wa zamani wa DRC leo anashtumu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kumnyang'anya mali zake na hivo kulipwa fidia.

Jean-Pierre Bemba anaomba fidia ya euro milioni 26 kwa miaka yote hiyo alikuwa gerezani akisema alifanyiwa unyonge kutokana na kutafsiri sheria vibaya, madai ambayo ofisi ya mashitaka ya ICC inapinga. Lakini kwa fedha hizo, kuna euro milioni 42, ambazo anasema ni fidia kutokana na uharibifu wa mali zake.

Wakati wa kukamatwa kwake, ICC iliomba nchi kadhaa kuzuia mali zake: nyumba ya kifahari na ndege aina ya Boeing 737 huko Faro nchini Portugal, akaunti za benki ikiwa ni pamoja na baadhi ya ndege na ndege sita nchini DRC za shirika lake la ndege.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.