Pata taarifa kuu
LIBYA-UN-MAPIGANO-USALAMA

Umoja wa Mataifa waomba kusitishwa kwa mapigano kwa wiki moja Libya

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kwa wiki moja kwa ajili ya kusafirisha misaada ya kibinadamu nchini Libya, ambapo majeshi ya Marshal Khalifa Haftar na yale ya Serikali ya Umoja wa kitaifa (GNA) yanapigana kudhibiti mji wa Tripoli.

Gari ya jeshi la serikali ya Libya, Ain Zara, Tripoli, Libya, Aprili 25, 2019.
Gari ya jeshi la serikali ya Libya, Ain Zara, Tripoli, Libya, Aprili 25, 2019. REUTERS/Hani Amara
Matangazo ya kibiashara

Mapegano hayo sasa yamedumu mwezi mmoja, huku wakaazi wa maeneo jirani ya mji huo wakiendelea kuyatoroka makaazi yao.

Katika taarifa, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (Manul) umeomba pande zinazohasimianakusitisha mapigano kuanzia mapema alfajiri Jumatatu hii Mei 6, 2019, tarehe iliyofikiwa ambayo inaendana na mwanzo wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Pande mbili zinazokinzana hazijatoa maelezo yoyote kuhusiana na wito huo wa Umoja wa Mataifa.

Makombora yaliendelea kusikika usiku kucha kusini mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli, ambapo majeshi ya Haftar yanatafuta kuvunja ngome za wanamgambo wanaounga mkono serikali ya Umoja wa kitaifa (GNA).

Mapigano yamesababisha watu 50,000 kuyatoroka makaazi yao, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.