Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-HAKI

Ndugu wa Bouteflika na maafisa wawili wa zamani wazuiliwa Algeria

Ndugu wa aliye kuwa rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, na maafisa wake wa karibu wa zamani wanaendelea kusakamwa na vyombo vya dola nchini Algeria.

Saïd Bouteflika (kulia) na kaka yake, rais wa zamani Bouteflika, Algiers, Aprili 10, 2009.
Saïd Bouteflika (kulia) na kaka yake, rais wa zamani Bouteflika, Algiers, Aprili 10, 2009. Reuters/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Said Bouteflika, mdogo wa Abdelaziz Bouteflika, amewekwa kizuizini na jaji wa mahakama ya kijeshi siku ya Jumapili (Mei 5). Wakuu wawili wa zamani wa idara ya upelelezi waliokamatwa Jumamosi pia wamewekwa jela.

Picha za watu hao zilioneshwa kwenye televisheni ya serikali Jumapili mchana. Saïd Bouteflika, ndugu wa Abdelaziz Bouteflika, Mohamed Médiene, mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi, na Athmane Tartag, ambaye alichukuwa nafasi yake hadi Abdelaziz Bouteflika alipotimuliwa madarakani, wote wanazuliwa na utawala mpya nchini Algeria.

Jaji wa mahkama ya kijeshi ameamuru watu hao wawekwe rumande.

"Kwa sababu za uchunguzi, mwendesha mashitaka wa kijeshi (...) amemuomba jaji wa mahakama ya kijeshi anayehusika na uchunguzi kuanza utaratibu wa uchunguzi, na baada ya kushtakiwa, jaji alitoa hati za watu hao watatu kukamatwa na kuwekwa jela", taarifa ya ofisi ya mwendesha mashitaka wa kijeshi imebaini.

Wanashutumiwa "kula njama za kuipindua serikali na kuhatarisha usalama wa uongozi wa jeshi". Mashtaka yanayofanana na yale yaliyotolewa na Mkuu wa jeshi Ahmed Gaid Salah wakati wa hotuba zake katika wiki za hivi karibuni. Hii inathibitisha kuwa ni hatua mpya katika mkakati wa kiongozi huyo wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.